4/10/2022

Ndege ya mizigo Aina ya Boeing ya DHL, imepata Ajali na Kukatika Vipande Viwili


Ndege ya mizigo aina ya Boeing 757-200 inayomilikiwa na Kampuni ya Usafirishaji ya DHL, imepata ajali mbaya kwa kukatika vipande viwili ilipotua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Juan Santamaria uliopo San José, nchini Costa Rica.

Mamlaka ya usafirishaji wa anga nchini humo imetoa taarifa kuwa ndege hiyo ilikuwa inaelekea Guatemala ikitokea uwanjani hapo, lakini baada ya dakika 25 ikiwa angani rubani wa ndege alipiga simu ya dharura na kuomba kurudi tena ili atue uwanjani hapo.

Hakuna taarifa za vifo kutokana na ajali hiyo ya kutisha! katika kipande hiki cha video kinaonesha ndege hiyo ikiwa imekatika vipande viwili huku juhudi za uokoaji zikiwa zinaendelea.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger