4/13/2022

Orlando Pirates Wataja Siku ya Kutua Nchini Alhamisi kwa Ajili ya Kuwawinda Simba

Nafasi za Ajira Jiunge Group la Telegram la AJIRA YAKO Kwa Kubonyeza >> HAPA
UONGOZI wa klabu ya Orlando Pirates umeweka wazi kuwa utatua nchini Alhamisi au Ijumaa tayari kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao wa kwanza wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Simba.

 

Mchezo huo unatarajiwa kufanyika Aprili 17 katika Uwanja wa Mkapa ambapo Orlando Pirates watakuwa wageni wa Simba katika robo fainali hiyo ya kwanza.

 

Akzungumza na Championi Jumatano, Ofisa Mtendaji wa Orlando Pirates, Floyd Mbele alisema kuwa mara baada ya kumaliza mchezo wao wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini uliopigwa jana wataangalia uwezekano wa kuondoka siku hiyo au kesho yake jambo ambalo litawafanya kufika Tanzania kati ya Alhamisi au Ijumaa tayari kwa maandalizi ya mchezo wao na Simba.

 

“Tukimaliza mchezo wetu wa ligi kuu ndio tutafahamu tutaondoka siku hiyo au kesho yake hivyo uhakika mzuri wa sisi kufika Tanzania ni kati ya Alhamisi au Ijumaa tayari kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu dhidi Simba.

 

“Malengo yetu yalikuwa ni kufika mapema Tanzania ili tuweze kuweka mipango yetu vizuri na kuzoea hali ya hewa lakini imeshindikana kutokana na kubanwa na ratiba ya michezo ya ligi kuu, lakini tunaimani kila kitu kitakuwa sawa,” alisema kiongozi huyo.

Stori na Marco Mzumbe
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger