Ticker

6/recent/ticker-posts

Pablo, Kapombe Wadai Orlando Anakufa, Mashabiki Wajae kwa Mkapa

 Habari Kama Hizi Zinapatikana UDAKU SPECIAL App, Download HAPA Bure: Link here>>>
KOCHA wa Klabu ya soka ya Simba Pablo Franco Martin amesema kwa upande wao kama timu wapo vizuri kuanzia benchi la Ufundi na wachezaji kwa ujumla.

Katika mahojiano yake na Waandishi wa Habari mapema asubuhi hii Kocha Pablo ametoa rai kwa mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi waujaze uwanja huo wa Benjamin Mkapa siki ya kesho ili kuwasapoti wachezaji katika mchezo huo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Pablo amesisitiza kuwa ni wazi klabu ya Simba imekuwa na rekodi nzuri inapocheza nyumbani kwahiyo wachezaji na timu kwa ujumla wanakila sababu ya kutumia faida ya uwanja wa nyumbani na kuhakikisha wanashinda pambano hilo.


                                 Mlinzi wa Kulia wa Klabu ya Simba Shomari Kapombe
Naye Beki wa Kulia wa Simba Shomari Kapombe ambaye aliambatana na kocha wake katika mkutano na waandishi wa habari amesema wachezaji wamejiandaa vizuri na wapo tayari katika kupata ushindi kwa mchezo wa kesho japo amekiri mchezo utakuwa mzuri na mgumu kwa timu zote mbili.


 
Klabu ya Simba inatarajiwa kucheza na Orlando Pirates ya nchini Afrika Kusini katika mchezo wa kufuzu wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam Jumapili ya Aprili 17 mwaka huu.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

________________________________

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments