Simba SC Waondoka Dar, waifata Orlando Pirates

 


Klabu ya Simba SC imeondoka Dar es salaam leo asubuhi Aprili 22, 2022. Kuelekea nchini Afrika Kusini ambako itacheza mchezo wa robo fainali wa mkondo wa pili ya kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Orlando Pirates.

Wekundu wa msimbazi ambao ni wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye michuano ya vilabu barani Afrika wanaelekea kwenye mchezo huu wakiwa na faida ya kuongoza bao 1-0. Ushindi ambao walipata kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa Aprili 17, 2022. Katika dimba la Benjamini mkapa Dar es salaam bao pekee ambalo lilifungwa na Shomari Kapombe kwa kwaju wa penati.


Kikosi cha Simba kimeondoka leo ikiwa tayari kwa mchezo huo wa mkondo wa pili utakaochezwa katika dimba la Orlando jiji Johannesburg. Na Simba itahitaji matokeo ya sare yoyote ile au ushindi ili kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hii.


Mwamuzi wa kati wa mchezo huo tayari ameshajulikana ni Bernard Camille kutoka nchini Ushelisheli (Seychelles).

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad