4/22/2022

Tanroads Yatoa Tamko, Daraja la Tanzanite Kufungwa Kupisha MatengenezoDaraja la Tanzanite linatarajiwa kufanyiwa marekebisho kuanzia Jumamosi hadi Jumapili
WAKALA wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Dar es salaam umetoa taarifa kwa Watumiaji barabara inayokwenda moja kwa moja hadi Daraja la Tanzanite kuwa Daraja hilo linatarajiwa kufanyiwa maboresho kadhaa  ya miundombinu hivyo barabara hiyo itafungwa kuanzia Jumamosi ya April 23, 2022 saa 12 asubuhi na kufunguliwa Jumapili April 24, 2022 saa 12 jioni.

“Katika kipindi chote cha maboresho ya Daraja hili vyombo vya moto pamoja na watembea kwa miguu hawataruhusiwa kupita katika Daraja kwasababu za kiusalama.”


Watumiaji wa vyombo vya moto wameaswa kutumia njia mbadala
“TANROADS Mkoa wa Dar es salaam inawashauri watumiaji wa Daraja hilo kutumia barabara mbadala ya Kaunda na Ali Hassan Mwinyi wakati wa maboresho husika

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger