4/10/2022

Uagizaji mafuta ya Urusi waongezeka MarekaniUagizaji mafuta ya Urusi waongezeka Marekani
Kiasi cha uagizaji wa mafuta ya Urusi kuingia Marekani kimeongezeka kwa asilimia 43 kutoka Machi 19 hadi 25, ikilinganishwa na wiki iliyopita, kwa mujibu wa ripoti mpya ya Utawala wa Habari za Nishati (EIA).

Takwimu zilizochapishwa na taasisi hiyo ya Kimarekani, zimesema taifa hilo liliingiza wastani wa mapipa 100,000 ya mafuta ghafi kutoka Urusi kwa siku.

Uagizaji ulikuwa umesimamishwa wakati wa wiki ya Februari 19 hadi Februari 25. Hata hivyo, mwanzoni mwa Machi, usambazaji wa kila wiki wa mafuta ya Urusi ulifikia kiwango cha juu cha mapipa 148,000 kwa siku.

Hatua hiyo inakuja licha ya Rais wa Merekani, Joe Biden kutia saini agizo kuu mnamo Machi 8, kupiga marufuku uagizaji wa nishati kutoka Urusi na uwekezaji mpya katika sekta ya nishati ya Urusi.


 
Wizara ya Fedha ya Marekani imeweka hadi Aprili 22 kama ukomo wa shughuli za uagizaji wa mafuta, bidhaa za mafuta, LNG, na makaa ya mawe kutoka Urusi.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger