Video ya Pasta Akipaa Mbinguni Yatetemesha Mitandao ya Kijamii
Katika video hiyo, mtumishi huyo wa Mungu anaonyesha akibebwa juu kwenye dari ya kanisa
Kisha anavutwa juu na kile kinaonekana kuwa kamba huku waumini wakiimba nyimbo za kusifu
Video hiyo imezua hisia mseto mitandaoni wengi wakitaja tukio hilo kama siku za mwisho
Video moja inayosambaa kama moto ikimuonyesha mchungaji kanisani akidaiwa kupaa mbinguni imezua mjadala moto katika mitandao ya kijamii.

Video ya Pasta Akipaa Mbinguni Yatetemesha Mitandao ya Kijamii
Katika video hiyo, mtumishi huyo wa Mungu anaonyesha akibebwa juu kwenye dari ya kanisa.
Katika video hiyo, mtumishi huyo wa Mungu anaonyesha akibebwa juu kwenye dari ya kanisa na kuvutwa juu kile kinaonekana kuwa kamba huku waumini wakiimba nyimbo za kusifu.

Japo haijabainika tukio hilo lilishuhudiwa wapi, inaidiwa ni kutoka kwa moja ya makanisa bara Afrika.

Maoni ya wanamitandao

Wanamtandao walikuwa na haya ya kusema

Little Brian: "Ukristo uliondoka Israeli kama familia, ukaja Roma kama dini, ukaenda Uingereza kama siasa na ukaishia Afrika kama biashara."


 
Halligan Agade: "Yesu Kristo alitangaza kwamba kutakuja wakati ambapo MANABII WA UONGO watakuwa wengi. Watawadanganya hata walio wateule. Kwa kweli huu ni uthibitisho."

Malaika Kimani: "Na nina hakika baadhi ya makutaniko yake wanasali kwa ndimi kwa kuguswa na kuhamia kwake mbinguni hii dunia ni Jupiter."

Michael Kip Lagat: "Bora asirudi Tena aende kabisa pengine kama wafuasi wake ni wajinga."


Tazama video hiyo hapa

https://www.facebook.com/NairobiJournalNews/videos/1148162539319234
Pasta aoa wake wanne siku moja katika harusi ya kufana
Katika taarifa nyingine ya kutamausha kuhusu dini, Tuko.co.ke iliripotia kumhusu mchungaji Zagabe Chiluza, mwanamume kutoka mashariki mwa Congo, alizua gumzo baada ya kuoa wake wanne.

Mchungaji huyo mwenye wake wengi aliwaoa wanawake hao wanne, wote mabikira, katika sherehe ya harusi ya kupendeza mwaka mmoja uliopita.

Alikuwa ameoa mke wa kwanza kabla ya kuoa hao wanne, akidai kuwa alipata wazo la kuwa na wake wengi kutoka kwa Biblia, akitumia Yakobo, ambaye alikuwa na wake wanne, kama mfano.

"Nimefurahi kuwa na wake watano. "Yakobo alikuwa na wake wengi Lea na Raheli, kisha Bilha na Zilpa ... wake wanne kwa mwanamume mmoja," alisema," Mchungaji Zagabe alisema wakati wa harusi yake


 
Mtumishi huyo wa Mungu aliyejaa majivuno alisema wanaume kutoka katika kanisa lake huoa mabikira pekee, akiwahimiza wengine kuoa wake wengi.


______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad