Ticker

6/recent/ticker-posts

Waziri Innocent Bashungwa Atoa Agiza zuio la Boda boda dar

 Habari Kama Hizi Zinapatikana UDAKU SPECIAL App, Download HAPA Bure: Link here>>>


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa @innocentbash amemuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla kusimamia usitishwaji wa zuio la bodaboda na bajaji kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Bashungwa amechukua hatua hiyo kufuatia uamuzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam la kupiga marufuku bodaboda na bajaji kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam isipokuwa maeneo yaliyoanishwa.

"Bila shaka nia ni njema, ila dosari ipo kwenye handling (kushughulikia) ya jambo lenyewe, Serikali yetu ya awamu ya sita inatambua na kuthamini ajira za vijana wetu za bodaboda na bajaji kuwa ni ajira rasmi na wanajipatia riziki na familia zao"

"Namuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Amos Makalla kusimamia usitishwaji wa zuio hilo ili kutoa nafasi ya kufanya tafakuri zaidi."

Tangazo la kusitisha vyombo hivyo vya usafiri kuingia katikati ya Jiji lilitolewa jana April 20,2022.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

________________________________

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments