4/21/2022

Steve Nyerere "Mama Ametuheshimisha Bongo Movie Kimataifa"Steve Nyerere, msanii wa Bongo Movie ambaye mara nyingi amekuwa mstari wa mbele kuitetea sanaa, ametoa pongezi kwa Rais Samia kwa kuiheshimisha Bongo Movie kimataifa.

Kupitia akaunti yake ya Instagram,
@stevenyerere2 ameandika:

"Kwanza nimpongeze Mh Rais kwa Kitendo tu cha kutamka Bongo Movie kwenye ROYAL TOUR, nadhani ni jambo kubwa na fahari kwa wacheza movie wa TANZANIA. Nimeona amekaa na MAPRODUCER wakubwa wa movie duniani na mara kwa mara nimesikia akiwaambia mnaweza kuja kucheza movie nyumbani mkishirikiana na wasanii wa TANZANIA. Kitendo cha Mh. Rais kuipa nafasi tasnia hii mdomoni kwake na kuitaja hili si jambo dogo, Tunafahamu soko la movie Marekani 🎬 🎞 πŸŽ₯ 🎦 lilivyokuwa juu kuliko taifa lolote lile. Tunaamini fursa hii kama itafanyiwa kazi basi naona kabisa ni jinsi gani wasanii wetu watakavyopeperusha bendera yetu ya Tanzania na kuitangaza TANZANIA kwenye sekta ya movie. Hili jambo tulicheleweshwa sana kama lingefanyika tangu miaka ya nyuma nathubutu kusema katika ukanda wa Africa 🌍 Tanzania ina wasanii wazuri na wenye uwezo mkubwa tatizo moja tu tulikosa na ambalo Mh Rais SAMIA Suluhu Hassan leo analifanya ni kutupigia debe ili tufike kule panapostahili. Niwaombe wasanii wenzangu wote tushirikiane tuungane kwenda na Mh. Rais katika kuhakikisha tasnia yetu inafika pale panapostahili...

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger