5/23/2022

Ali Kamwe "Mambo 10 nilioyaona BIASHARA vs YANGA"

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

 


1: CLASSIC MATCHπŸ™Œ KILA TIMU IMEPATA ILICHOSTAHILI. ALAMA 1 MUHIMU kwa safari ya Ubingwa kwa Yanga. ALAMA 1 kwa Biashara United kwenye Harakati za Kubaki Ligi Kuu


2: TACTICALLY.. Well done kwa Kocha wa Biashara, Vivier Bahati. Operation ya 3-5-2 kwa kuanza na Holding Midfielder wawili, James Mwashinga na Ndunguri huku Zigah na Atupele wakidrop kwenye 'Half Spaces' kuliwapa mzigo viungo watatu wa mwanzo wa Yanga.. Kivipi?


3: YANGA walianza na 4-3-3.. Mauya akicheza chini ya Farid na Feisal. Eneo hili Biashara walikuwa na wwanne muda mwingi wa mchezo. Vita ikawa 3v4! BACK 3 YA BIASHARA Ikacheza kwa utulivu kiasi dhidi ya Mayele


4: Kwa ratiba ilivyo, Umuhimu wa Mchezo wa nusu Fainali.. Unaelewa kwanini NABI alifanya Rotation kubwa kwenye kikosi chake! Lakini Tactically, Nafikiri 'Sub' ya Makambo ilitakiwa iwahi kidogo, Yanga waswitch kutoka kwenye 4-3-3 kwenda kwenye 4-2-4! 


5: MAYELE.. TOP STRIKER! Anaweza asiwe na mechi nzuri kwa dakika 70  Lakini nusu nafasi atakayopata dakika inayofata akakudhuru! Vita ya Kiatu cha Ufungaji bora zinazidi kukolea


6: Yassin Mustapha anatakiwa kurudi kwenye kioo kujitazama mara mbili. Benchi linaweza kuwa sababu ya kushuka kwa kujiamini kwake Lakini hizi dakika anazopewa alitakiwa kuthibitisha mengi sana


7: AMBROSE AWIO..πŸ™Œ WHAT A PLAYER. Mimi ni shabiki yake mkubwa sana. Kama 'wing back' ni hatari sana. Anajua vyema kuhesabu hatua za beki kabla hajafanya maamuzi ya pasi yake ya mwisho


8: 'Well Done' COLLINS OPARE. Sub yake ilikuja kwa wakati sahihi sana uwanjani. Uwezo wake wa kukontroo mpira.. Spidi na movements zake ziliwapa wakati mgumu sana mabeki wa kati wa Yanga


9: HESHIMA KWA KAYOKO. Haiwezi kuwa kwa asilimia 100 Lakini ANAFANYA VYEMA SANA. Anafika kwa wakati kwenye matukio na Ana mamlaka kwenye uwanja. Tunachukia kwa sababu wengi hatujazoea Maamuzi ya FAIR.


10: Well Done Mshery. Save bora sana ya mechi kutoka kwenye mikono yake! Kazi nzuri kwa Mgore pia. Alikuwa mtulivu sana kwenye kufata mipira ya krosi


Nb: Mayele katetema, Imetosha πŸ˜ƒ

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger