Ticker

6/recent/ticker-posts

Aliyefanya Operation ya Nyusi Ili Awe Mrembo Afunguka Kilichompata


Mrembo huyo kwa jina la Crystal(37) amepatwa na mshtuko baada ya kwenda kufanya sajari ya nyusi azidi kuwa mzuri ila matokeo yamekuwa hayo nyusi zimekuwa kama kichaka cha masinzi hadi anakimbiwa na mtoto wake wa miaka 3 kwa kuogopa muonekano wake huo mpya


Mrembo huyo amesema sababu ya ubize wa kazi na kuwa mama alikuwa hana muda wa kutengeneza nyusi zake kila siku kwani ni nyembamba na hazijajaa vizuri ndio akaona akafanyiwe upasuaji kabisa zikae sawa moja kwa moja ambapo ametumia dola $340 ambazo ni sawa na laki 790,000 za Kibongo


Kwasasa anajuta kila akijitazama kwenye kioo haamini kuwa ni yeye anataka uzuri wake wa zamani ila ameambiwa itachukua takribani mwaka angalau awe sawa kwani wakati alipokuwa akifanyiwa sajari na kuwekewa vitu husika alivuja damu mara mbili nyakati tofauti tofauti

Amesema hakutarajia kuwa hivyo kwani mategemeo yake ilikuwa azidi kuwa mwenye mvuto


Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments