5/05/2022

Hili Ndilo Gauni Ghali Kuliko Yote Duniani...Kim Kardashian Ilibidi Ajipunguze Mwili Ili Alive Kwa Dakika Chache


Gauni hilo lililovaliwa na Kim Kardashian(41) juzi katika tamasha kubwa la Met Gala, liliwahi kuvaliwa miaka 60 iliyopita na mwigizaji mashughuli Marilyn Monroe wakati alipohudhuria birthday ya Rais wa 35 wa Marekani John F. Kennedy mwaka 1962

Gauni hilo mbunifu wake kwa wakati huo alilipwa dola $1440 ambazo kwasasa ni zaidi ya milioni 3.3 za Kibongo


Mwaka 1999 gauni hilo lilipigwa mnada na kuuzwa kwa zaidi ya dola $1 milioni ambazo ni zaidi ya bilioni 2.3 za Tanzania kwasasa

Kwa mujibu wa Vogue, mwaka 2016 gauni hilo lilipigwa mnada tena na kuuzwa kwa dola $4.8 milioni ambazo ni zaidi ya bilioni 11 za Tanzania kwasasa. Kisha gauni hilo likapelekwa kwenye jumba la makumbusho la Ripley kuhifadhiwa. Ndilo hadi sasa linashikilia rekodi ya dunia kwa kuwa gauni ghali zaidi kuuzwa katika mnada


Kim Kardashian akihojiwa amesema miezi kadhaa kabla hakujua atavaa nini ndipo alipokumbuka gauni la Merilyn Monroe akawasiliana na makumbusho ya Ripley ambapo alikubaliwa kulivaa kwa masharti makali

Kwanza Kim alipewa copy ya gauni hilo ajaribu Kama litamkaa vizuri, copy ilimkaa vizuri, baadaye gauni halisi lilisafirishwa kwa ulinzi mkali kwenye ndege maalum binafsi kupelekewa Kim lakini kwa bahati gauni halisi halikumtosha Kim akamwaga chozi kwa uchungu


Kim hakutaka akose nafasi ya kuvaa gauni hilo ilimbidi awe kwenye diet kali ya kupunguza mwili kwa mwezi mmoja, alisitisha kula vyakula vyenye sukari na vyakula vya wanga ili mwili usiongezeke. Alikuwa anakula zaidi mboga za majani na protein ambapo safari hii gauni lilimtosha. Lakini alisimamiwa na ulinzi mkali Kama wa jeshi ili mapaparazi wasimpige picha kabla ya tamasha. Na pia Kim hakutakiwa kula Wala kukaa akiwa kavaa gauni Hilo halisi ili kuepuka kuliharibu

Hata hivyo, Kim aliruhusiwa kulivaa gauni hilo ukumbini kwenye Met Gala kwa dakika chache tu baada ya kupigwa picha rasmi na mapaparazi, Kisha akalivua na kupewa copy ya gauni hilo. Hadi ukumbini kwenye Met Gala alipewa wasimamizi wa makumbusho ya Ripley .


Marilyn Monroe alifariki 1962 akiwa na miaka 36 lakini hadi sasa bado jina lake linaingiza pesa nyingi kila mwaka kwani makampuni bado yanatumia hadi sura yake kibiashara

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger