Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
TIMU ya Liverpool imefanikiwa kutwaa Kombe la FA England baada ya miaka 16 kufuatia ushindi wa penalti 6-5 timu hizo zikitoka kumaliza dakika 120 bila kufungana Uwanja wa Wembley Jijini London.
Waliofunga penalti za Liverpool ni James Milner, Thiago Alcântara, Roberto Firmino, Trent Alexander-Arnold, Diogo Jota na Konstantinos Tsimikas, huku Sadio Mane pekee akikosa mkwaju wake ukiokolewa na kipa Msenegal mwenzake, Édouard Mendy.
Upande wa Chelsea waliofunga ni Marcos Alonso, Reece James, Ross Barkley, Jorginho na Hakim Ziyech huku César Azpilicueta na Mason Mount wakikosa.
LOVE STORY YA UTANIKUMBUKA NEYLA Ipo tayari ni maandishi na Sauti !, Kuisoma yote Bonyeza HAPA Lipia tsh 1000 Tu mtandao wowote,au Tembelea www.makapedia.com