Mke wa Sugu Asimulia Alivyopata Mtoto Kimaajabu Baada ya Hospitali Kumwambia Hatoweza Kushika Ujauzito

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


USHUHUDA WANGU

Kwa walionifuatilia siku nyingi walijua mimi Happiness sina uwezo wa kushika ujauzito kitu ambacho kilikuwa si ukweli. Mnamo mwaka 2017 niliamua kufanya vipimo kuangalia kama mfumo wangu wa uzazi uko sawa chini ya Dr Shafiq na kila kitu kilikuwa OK. Lakini hata hivyo sikuweza kushika ujauzito kwa muda mrefu. 

Hiyo picha hapo juu ni 2018 muda mfupi baada ya kutoka kwenye oparation ndogo kuangalia tena mfumo wangu wa uzazi katika hospital kubwa hapa Dar. Siku hii nilipoteza matumaini baada ya kupokea majibu yangu kuwa sitaweza kuzaa kawaida ni lazima nipandikize maana mirija imeziba... Nililia na kutetemeka sana nikajiuliza why mbona 2017 tu nilikuwa OK why sasa?

Anyways, Doctor akaniambia wao hapo hospital wana pandikiza so tuanze process mwezi wa 8 hapo it was July ili hadi kufikia Sept tayari ntakuwa mjamzito. Nilimpigia Joseph wangu simu nikamueleza kiufupi huku nikilia sana.. akaniambia kesho nakuja Dar tuongee mammy don't worry, wakati huo alikuwa Dodoma.


Madaktari wakanisihi sana kunituliza na kunipa moyo. Nakumbuka akaja dada yangu Judy nikamweleza majibu yangu, akaniambia mdogo wangu tuliaa tuyakatae haya majibu kwa jina la Yesu tena tutoke hapa hospital! Haya maneno yalinipa nguvu ya Ajabu. Basi Joseph wangu alipokuja home tukaongea sana usiku huo alinipa moyo sikutarajia.Aliniambia Happy naamini huna tatizo moyo wangu haujashituka ondoa hofu na hata kama ni kupandikiza tutapandikiza hata Marekani ukitaka. 

Lakini pia alinipa mifano mingi ya mastar wa ulaya waliozaa kwa kupandikiza kwamba ni kawaida tu ila niliendelea kulia sanaa usiku ule nikamwambia daddie kwanini nisipate ujauzito kawaida? Huku nikilia kwa uchungu. Akaniambia mimi nipo pamoja na wewe kwa hali yeyote ile. 


Kwakweli baada ya hapo nilipata nguvu mpya kabisaa maana kama Joseph wangu kaahidi kuwa nami kwa hali zote ya nini nilie tena? Maana wanaume wengi huwa ni tatizo. 

Lakini niseme tu mume wangu alinisaidia sana kutuliza akili nika relax. Baada ya siku kadhaa nilikutana na Mtumishi, dada Vaileth ambae ni rafiki wa wifi yangu Sponsa. Akaniambia utazaa Happy hakuna cha kupandikiza wala nini huyu ni shetani tu tutashinda kwa kuomba na kufunga. 


Tukakubaliana hakuna kurudi tena hospital pale.Basi dadangu Mtumishi akaniongoza wapi nipitie kwenye bible kusoma neno la Mungu na kuomba jamani bible imeandika kila kitu ni vile tu wengi hatufahamu neno but ukipata wa kukuongoza utajionea, nilikutana na neno hakuna tasa wala mgumba aisee 😭😭nilijua kuomba kipindi hiko.

Hiyo ilikuwa July hapo bado kufika August pale hospital walinipigia nirudi kwajili ya maandalizi ya kupandikiza. Nikawa nawapiga chenga bwana. Huku nikiendelea na kufunga na kuomba. Nakumbuka kuna siku nilimwambia Mungu sitaenda hospital wala sitatumia dawa yoyote ya mganga maana nilishaweka nadhili na Mungu wa Israel miaka mingi iliyopita kutokanyaga nyumba ya mganga hata ikitokea niumwe vipi bora  nife lakini siyo kwenda kwa mganga. 

Jaribu likanijia wapo walionishauri kwenda kwa waganga sijui wataalam mara bibi sijui kwa babu😀sijui nani lakini nilimkumbusha Mungu kuwa wewe pekee ndiyo mganga wangu na ndiye daktari wa madaktari wote na nikamwambia nitafunga hadi utakaponijibu km kufa nife nikiwa nimefunga kwajili ya kukuamini Yehova! Lakini kamwe sitavunja agano langu kwako!🥲 Neno moja nililolishika ni Kutoka 23:25-26 Nanyi mtamtumikia BWANA Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako.

 Hapatakuwa na mwenye kuharibu MIMBA wala aliye TASA katika nchi yako na hesabu ya siku zako nitazitimiza. Nilimlilia Mungu na kuweka nadhiri kama Hannah alivyofanya kwenye kitabu cha Samweli 1:10-11. Nikiwa bado kwenye kufunga na kuomba hapo ni September sasa, nikaona nimepitiliza mwezi lakini nikasema inawezakanaje nikawa mjamzito ghafla hivyo? Siku hiyo nikaingia ofisini Mlimani city pale asubuhi nikasema leo nitajipima iwe isiwe nakumbuka hadi toilet niliyoingia siku ile ili kujipima,nikachukua kifuniko cha maji nikanunua UPT pale JD Pharmacy,basi nikiwa toilet nikamwambia Mungu eeh Mungu wangu kama nitajikuta ni mjamzito huu utakuwa ni MUUJIZA/miracle na huyu mtoto nitakupatia maana atakuwa muujiza wangu! 

Ile kujipima mistari 2 ikagonga paap!😀 Nilipiga magoti pale toilet sikujali wala nini! Nikainama NIKASUJUDU! mkojo ukanimwagikia😭nikatoka mbio nikaanza kupiga simu ya kwanza kwa Joseph hakupokea nikampigia dadangu kipenzi Mtumishi Vaileth akasema Haleluyah huyo ndiye Mungu asiyeshindwa! Akaniombea nikashikilia tumbo langu nikaamini! 🤰Nikamrudia Baba Shawn aisee ilikuwa furaha na kicheko daddie nimejipima nimekuta I'm pregnant wee nikaskia bonge la yoweee mara eti haraka nitumie pic ya hiyo UPT then toka ofisini nenda hospital now.. tena kama umevaa heels👠 zako uvue 🤣🤣 basi nikaendelea kuwajulisha watu wangu wa karibu wote walimsifu Mungu kwajili yangu!

Nikampigia Dr Shafiq akasema njoo hospital tupime mimi kufika nikawaambia mapokezi nipimeni vipimo vyote vya mama mjamzito🤣 wakati namngoja Dr mara nikakumbuka lazima nipime tena kuhakikisha kama kweli i'm preg nikawaambia  nipimeni na UPT wakasema kwani si ni mjamzito umesema?nikawaambia nataka kuhakikisha nimejipima mwenyewe yani nilikuwa na imani iliyozidi milima😀 Hata nilipo enda kwa ultrasound kuambiwa ninywe maji mengi ndo nakumbuka kumbe nilikuwa nimefunga!🤣

 Baada ya hapo ukawa mwanzo mpya na sikuogopa wala kujificha eti watu wasinione sijui vijicho sababu tayari nilijikabidhi mikononi mwa Mungu! Nilihamia kwa Dr Kaguta baadae coz ndoto yangu ilikuwa nijifungulie Aghakhan  pale pavilion pazurii 😀na ndipo nilijifungulia mtoto wangu kipenzi my miracle kid Shawn Joseph Mbilinyi! Hadi leo nakumbuka nilikuwa labor na baba yake na my sisters Judy na Sarah. Sitawasahau kwa ambavyo walihangaika na mimi siku ile.. pia niwashukuru wote ambao siwajui ila mliniombea! Mwanamke mwenzangu au binti usikubali maneno mabaya utakayotamkiwa kuwa eti wewe ni mgumba huzai usiyapokee yakatae kwa jina la Yesu yakemee ukiyakubali shetani atajitwalia utukufu hapo! Mungu na neno lake ndio wenye usemi wa mwisho kwenye maisha yako.

 Usivunjike moyo kuwa na imani wala usihuzunike! Wakati naomba nilimsihi Mungu anipe mtoto wa kiume na wote tulitamani baby boy! Babake alimuita Shawn kabla hajazaliwa! Shawn means A gift from God! Kwa Mungu yote yanawezekana!🙏 SIFA na UTUKUFU tunamrudishia MUNGU wa Israel !🙏  
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad