5/08/2022

Mrembo Asukumwa Jela Miezi 6 kwa Kutoboa Kondomu za Mpenziwe Kupata MimbaMrembo Asukumwa Jela Miezi 6 kwa Kutoboa Kondomu za Mpenziwe Kupata Mimba
Mrembo Asukumwa Jela Miezi 6 kwa Kutoboa Kondomu za Mpenziwe Kupata Mimba.
Katika uamuzi ambao hakimu aliutaja kuwa wa "kihistoria," mshtakiwa alidaiwa kutoboa mashimo kwenye kondomu za mpenzi wake bila yeye kujua.

Sababu ya kitendo hicho cha uhalifu kinachojulikana kama "stealthing"(kutoa kondomu bila idhini ya mwenzako wakati wa ngono) ni kuwa mwanamke huyo alitaka kupata mimba kinyume na ridhaa ya mwanamume.

Deutsewelle inaripoti kuwa mwanamke huyo alikuwa katika mpango wa "marafiki wenye manufaa" na mwanamume mwenye umri wa miaka 42 ambaye alikutana naye mtandaoni mwaka wa 2021.

Aibu! Hedimasta Ajificha Baada ya Mwanafunzi Wake wa Zamani Kumchekelea Akiwa Kwenye Bodaboda
Kile ambacho kilikusudiwa kuwa uhusiano wa kawaida hata hivyo, kiligeuka alipoanza kuwa na hisia ya kimapenzi kwa mwanamume huyo.

Katika hatua iliyolenga kumnasa, mwanamke huyo alitoboa kwa siri mashimo kwenye kifurushi cha kondomu ambacho mwanamume huyo alikuwa nacho kwenye chumba chake.

Lakini mpango wake haukufaulu kwa sababu hakupata ujauzito na alikuwa amemjulisha mwanamume huyo kupitia WhatsApp kwamba alikuwa ameharibu kondomu zake kimakusudi.


Baada ya kukiri kwake, mwanamume huyo alimfungulia mashtaka ambapo aliungama kwamba alijaribu kumhadaa mpenzi wake.

Hata hivyo, kulikuwa na mkanganyiko mahakamani pale waendesha mashtaka walipotatizika kuafikiana kuhusu mashtaka mahususi ya kuwasilisha dhidi ya mshtakiwa.

"Tumeandika historia ya kisheria hapa leo," Jaji Astrid Salewski alisema wakati wa uamuzi huo.

Hukumu huo wa miezi sita kwa mwanamke huyo, ulitolewa katika mahakama ya kikanda katika mji wa Bielefeld magharibi mwa Ujerumani.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger