5/20/2022

Mwanamke Mwenye Sehemu Mbili za Uke Afunguka Shida Anazopitia

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

Mapya yaibuka...Mwanadada pichani kwa jina la Lenane ameibuka kuelezea hali isiyo ya kawaida ambayo amezaliwa nayo. Amesema amezaliwa na sehemu mbili za siri zote za kike(two vag*nas), pia amezaliwa na mifuko miwili ya uzazi, na pia amezaliwa na cervix mbili


Pia ameeleza kuwa kwa mwezi anapata hedhi mbili(two periods) lakini anashukuru periods zote mara nyingi hutokea kwa wakati mmoja isipokuwa nadra sana ndio hedhi hizo zaweza kupishana kidogo

Amesema kwa hali yake ni hatari kidogo kubeba mimba na labda ajifungue kwa njia ya upasuaji

Lakini pia kwa hali aliyonayo anaweza kubeba mimba mbili za wanaume tofauti kwa wakati mmoja ila hili litawezekana tu ikiwa mimba zote mbili zitatunga ndani ya wiki mmoja. Hata hivyo, amesema hiki si kitu anachowaza kukijaribu kufanya


Kwa ujumla amesema vitu vingi vinavyohusiana na mfumo wa uzazi ambavyo vinawatokea wanawake wengi mara moja kwa yeye vinatokea mara mbili kutokana na hali yake

Amejibu maswali mbalimbali aliyoulizwa na watu ambao walishtushwa na hali hiyo na amesema ameamua kuzungumza sasa kuhusu hali yake ili kujaribu kutoa elimu kwa watu ambao hawafahamu kuhusu jambo hilo
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger