5/02/2022

Mwanamuziki SUGU Afikisha Miaka 50

Nafasi za Ajira Jiunge Group la Telegram la AJIRA YAKO Kwa Kubonyeza >> HAPA
Leo Tarehe 1.5.2022 ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Sugu au unaweza muita @jongwe__ ambaye ametimiza miaka 50

Ukizungumzia muziki, amefanya mambo mengi makubwa kwakutengeneza historia hata nje ya muziki

Pia huwezi acha kueleza ni msanii wa kwanza wa Hip Hop kuwa Mbunge, Jimbo la Mbeya mjini huku akiwa ni Mpinzani kupitia chama cha Chadema

kama hukujua unajua @jongwe__ ndio msanii peke mwenye album nyingi Tanzania, hakuna yeyote anayemfikia

Mpaka sasa Sugu ana Album 10 ambazo ni Ni Mimi (1995), Ndani ya Bongo (1996), Niite Mister II (1998), Nje ya Bongo (1999), Millennium (2000), Muziki na Maisha (2001), Itikadi (2002), Sugu (2004)
Coming of Age-Ujio Wa Umri (2006) pamoja na VETO (2009). (Album)

Na kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika hivi "@jongwe__ JONGWE is 50 today...Feeling much BLESSED, MUNGU amekuwa MWEMA sana kwangu na NAMSHUKURU sana 🙏🏾 ... #TAITA #JongweForLife #TheDreamConcert"

Ni wimbo gani kutoka kwa @jongwe__ unaukubali ?


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger