5/08/2022

Rais Samia "Sasa ni Rukhsa Kwa Filamu ya Royal Tour Kuoneshwa Kwenye TV Zote Tanzania"


Rais Samia kwenye uzinduzi wa Filamu ya Royal Tour Dar es salaam leo amesema kwa sasa ni rukhsa kwa TV zote na Watu wote kuionesha Filamu hiyo baada ya uzinduzi wake wa mwisho kuhitimishwa leo.

"Tulianza uzinduzi Marekani, Arusha, Zanzibar na leo tunahitimisha hapa Dar es salama na kuanzia leo kama alivyosema Katibu Mkuu itakuwa rukhsa kwa TV zote na Watu wote kuionesha na iweze kuonekana na Watanzania wote"

"Nashukuru tumewaletea kitu kitakachobaki kuwa urithi kwa vizazi vya sasa na vijavyo na sio urithi tu wa kuangalia Filamu na kuburudika lakini pia kuutangaza utalii wetu kwa faida za kiuchumi na kijamii"

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger