5/11/2022

Rihanna Kuleta Bidhaa zake Afrika, Ataja Nchi Atakazo Ingiza, Tanzania Bila Bila


Mwanamuziki 'Rihanna' @badgalriri ametangaza rasmi kuanza kuingiza bidhaa zake za urembo zijulikanazo kama @fentybeauty na @fentyskin barani Afrika.

Rihanna ambaye amejikita zaidi katika masuala ya biashara kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni, katika taarifa yake kupitia ukurasa wake wa Instagram ameyataja mataifa ambayo yamepata bahati hiyo kuwa ni Botswana, Ghana, Kenya, Namibia, Nigeria, South Africa, Zambia na Zimbabwe.

Aidha, bidhaa hizo zitaanza kuingia kwenye mataifa hayo ya Afrika kuanzia Mei 27 mwaka huu. "Huu ni mwanzo tu" - ameeleza Rihanna ambaye anatarajia kujifungua hivi karibuni.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger