5/06/2022

Ripoti Kamili Kuhusu Rihana na Mchumba wake Kufunga Ndoa Hii Hapa


Mapema usiku wa jana Alhamisi ziliibuka taarifa kuwa A$AP Rocky na bibie Rihanna tayari wamechumbiana na Riri amekubali kuolewa, hii ni baada ya Rocky kuachia video ya wimbo wake mpya "D.M.B" ambapo kwenye video hiyo kuanzia dakika ya 3, Rocky na Rihanna wanaonekana wakiwa wamevalia meno ya bandia (Grillz) ambayo yamenakshiwa kwa dhahabu yakiwa na ujumbe “MARRY ME” kwa Rocky huku Rihanna naye meno yake yakiwa na maneno “I DO”.


Vyanzo mbalimbali vikubwa vya burudani vilitafsiri kitendo hicho nikwamba Rihanna amekubali ombi la kuolewa na Rocky ambaye wanatarajia mtoto wao wa kwanza hivi karibuni na kwenda mbali zaidi kwa kueleza wawili hao tayari wameshachumbiana.


Kwa mujibu wa TMZ, chanzo kimoja cha karibu na wawili hao kimeimbia tovuti hiyo kuwa taarifa za Rocky na Rihanna kuvishana pete ya uchumba sio za kweli kama ilivyodhaniwa baada ya kuonekana kwenye video hiyo. Chanzo hicho kimeeleza kuwa wazazi hao watarajiwa walitumia meno ya bandia (Grillz) na kuyapamba maneno yale (“MARRY ME” na “I DO”), kwaajili ya kujifurahisha tu na hakuna kingine.

✍️: @omaryramsey

#SNSEnt

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger