5/08/2022

RPC Tanga ataja chanzo ajali DC Korogwe Basila MwanukuziKAIMU Kamanda Polisi Mkoa wa Tanga, David Mwasimbo amesema chanzo cha ajali ya gari aliyopata Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Basila Mwanukuzi jana mkoani Tanga, ni uzembe wa dereva wake. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza na MwanaHalisi Online leo tarehe 8 Mei, 2022 Kamanda Mwasimbo amesema ajali hiyo ya gari imetokea jana tarehe 7 Mei, 2022 katika barabara ya Tanga-Segera eneo la Hale wilayani humo.


Amesema dereva wa Mkuu huyo wa wilaya alishindwa kulimudu gari hilo aina ya Toyota Land cruiser kutokana na mwendokasi hali iliyosababisha kupata ajali.

Amesema ndani ya gari hiyo mbali na dereva pamoja na Mkuu huyo wa wilaya pia alikuwapo kijana mmoja ambaye ni msaidizi wa Ofisi ya Basila.

Amesema dereva na kijana huyo wamepata majeraha madogo lakini Mkuu wa wilaya hiyo ya Korogwe kwa upande wake aliumia vidole vya mguu wa kushoto na shingo baada ya mkanda wa usalama ndani ya gari kumkaba.

Aidha, amesema hali za majeruhi wote zinaendelea vizuti na hadi sasa wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Tanga, Bombo.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger