5/20/2022

Ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania upo matatani

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPARais wa Uganda Yoweri Museveni akiwa na mwenzake wa Tanzania Samia Suluhu Hassan walipokutana katika ikulu ya Entebbe April 11, 2021
Rais wa Uganda Yoweri Museveni akiwa na mwenzake wa Tanzania Samia Suluhu Hassan walipokutana katika ikulu ya Entebbe April 11, 2021
Deutsche Bank imeripotiwa kwamba haitafadhili mradi mkubwa wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoina Uganda hadi Tanga, Tanzania.

Hii ni baada ya wanaharakati wa mazingira kuasilisha malalamishi kwamba ujenzi wa bomba hilo utapelekea watu kadhaa kukoseshwa makao, pamoja na kuvuruga maisha ya wanyama wa porini.

Shirika la habari la Reuters limeripoti kwamba benki hiyo kubwa ya Ujerumani imekumbana na shinkizo kubwa kutaka kueleza mkataba wake wa ufadhili wa mradi huo wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta, utakaogharimu kiasi cha dola bilioni 3.5.

Bomba hilo lina urefu wa kilomita 1,400, kati ya Uganda na Tanzania.

Benki ya Deutsche haijatoa taarifa kamili lakini kundi la kutetea mazingira la 350.org linapanga maandamano kupinga ufadhili wake katika siku zijazo.

Kundi hilo limesema kwamba wafadhili kadhaa wa mradi huo na mashirika ya bima yamejiondoa na sasa wanataka benki ya Deutsche kujiondoa.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger