Viongozi wa CHADEMA wanashikiliwa na Polisi mkoani Manyara

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Na John Walter-Babati.

Viongozi mbalimbali wa Kitaifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na wengine zaidi ya 18 wa wilaya ya Babati mkoani Manyara wamekamatwa na polisi Jumatano Mei 25,2022  na kupelekwa katika kituo cha Babati kwa mahojiano.

Mwenyekiti wa CHADEMA mjini Babati Edgar Mwageni, amethibitisha kukamatwa kwa viongozi hao, akisema kuwa waliokamatwa ni pamoja na Mwenyekiti wa baraza la Vijana Taifa John Pambalu.

Bw Mwageni  amesema viongozi hao walikamatwa wakiwa  wanazunguka kuzungumza na baadhi ya wanachama wao mjini Babati wakihamasisha juu ya kampeni yao ya Kitaifa ijulikanayo kama "Join the Chain".

Amesema siku ya Jumanne waliketi kikao cha ndani katika Ukumbi wa AVIT mtaa wa mji mpya na kuzungumza juu ya umuhimu wa Katiba mpya bila usumbufu wowote.


 
Haijulikani ni sababu ipi ilisababisha maaafisa hao kukamatwa  Lakini  kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo anasema huenda  walikamatwa kwa sababu ya mkusanyiko usiokuwa na kibali.

Kwenye Ukurasa wake wa Twitter Mratibu wa Uhamasishaji Baraza la vijana wa chadema Taifa (BAVICHA) Twaha Mwaipaya , ameandika "Tumekamatwa na polisi,tupo ofisi ya RPC mkoa wa Manyara,kosa ni kudai katiba mpya".

Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Manyara Benjamin Kuzaga amesema ni mapema kuzungumzia tukio hilo.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad