6/13/2022

Aliyetoka gerezani kwa huruma ya Rais amkata mapanga mama yake

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Polisi nchini Kenya katika Kaunti ya Kirinyaga inamsaka aliyekuwa mfungwa kwa amemuua mama yake kwa kumkatakata na mapanga.

Mwanamume huyo ni mmoja wa wafungwa 3908 wa makosa madogomadogo ambao walisamehewa na Rais Uhuru Kenyatta katika sherehe za siku ya Madaraka Juni 1, 2022.

Insemekana sababu za magombano yao ni kile kinachokisiwa kuwa ni mzozo wa shamba ambapo mwanamume huyo alimuua mamake kwa kumkatakata kisha kukimbilia mafichoni.

Mtuhumiwa huyo alimuua mama yake Grace Muthoni Ndambiri, bafuni katika kijiji cha Njoga mnamo Jumapili, Juni 12, na kukimbilia mafichoni.


 
Majirani ambao walifika kusaidia baada ya kusikia kelele za kuomba msaada walikuta mwanamke huyo mwenye umri mkubwa akiwa amelala kwenye kisima cha damu na kutoa ripoti polisi.

Mkuu wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Mwea Mashariki, Daniel Kitavi alisema kuwa maafisa wake walikuta mwili wa mama huyo ukiwa katika nyumba kuu, wakautoa na kuupeleka katika Makafani ya Kibugi.

“Mwanamke huyo alishambuliwa vibaya sana na alikuwa na majeraha mabaya ya kukatwakatwa kichwani,” Kitavi alisema.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger