Ticker

6/recent/ticker-posts

Bernard Morrison Arejea Dar, Awaaga Kitofauti Simba Kutambulishwa Yanga Agosti 15

Kiungo mshambuliaji wa Simba Mghana, Bernard Morrison.
KIUNGO mshambuliaji wa Simba Mghana, Bernard Morrison jana Jumanne alirejea nchini Tanzania huku akitumia njia kitofauti kuwaaga mashabiki wa timu hiyo.

Mghana huyo amerejea nchini akitokea nyumbani kwao Ghana alipokwenda kwa ajili ya mapumziko mafupi mara baada ya kupewa ruhusa kutoka kwa uongozi wa timu hiyo.

Kiungo huyo inaelezwa kuwa tayari ameshamalizana na timu yake ya zamani ya Yanga mara baada ya kufikia makubaliano ya kusaini kimyakimya mkataba wa miaka miwili.

Morrison huenda akatambulishwa Agosti 15, mwaka huu mara baada ya mkataba wake kumalizika Agosti 14 ikiwa siku moja kabla usajili wa wachezaji wa kimataifa kufungwa na Caf.


 
Nyota huyo asiyeishiwa vituko, mara baada ya kutua nchini aliandika ujumbe wa kuwaaga mashabiki wa timu hiyo, kupitia moja ya kurasa zake za kijamii uliosomeka hivi: “Mara nyingi tunakatishwa tamaa na wale tunaowapenda na kuwaamini.

“Lakini wacha nifanye hadithi yangu kuwa fupi na rahisi, nahitaji vipande 100 vya jezi za Simba kutoka kwa mashabiki waaminifu ili niwape marafiki na familia nchini Ghana.

“Hii ni kutokana na nyinyi mashabiki kuniaga kwa sababu nilikatishwa tamaa ikiwa nitaendelea kusubiri kupata moja kutoka kwa klabu yangu. Tafadhali andika jina lako nyuma na namba 3 na atakayekuwa tayari kunipatia napatikana Sea Breeze, Mbezi Beach na anaweza kunipigia kwa namba hii ya simu 0745460326, Nimefika Dar. Nitawakumbuka wote.”

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments