Ticker

6/recent/ticker-posts

"Nitakuwa mke chini yako" Diva thee Bawse amuomba msamaha mumewe akitaka warudiane"Diva atakua Diva akiwa nje, ila kwako nitakua mke mbele ya mume wake @sheikh_abdulrazak_salum,” - Diva thee Bawse.

"Diva atakua Diva akiwa nje, ila kwako nitakua mke mbele ya mume wake @sheikh_abdulrazak_salum,” - Diva thee Bawse.


Ndoa ya mtangazaji wa kituo cha redio cha Wasafi, Diva thee Bawse imepatanyufa kubwa kwa takribani mwezi mmoja sasa, miezi mitatu tu kabla yake kufunga ndoa takatifu na Sheikh Abdulrazak Salum.

Inadaiwa kwamba wawili hao walianza kutofautiana baada ya Sheikh huyo ambaye ni mja wa dini kwa asilimia kubwa kumtaka mkewe Diva kuvaa mavazi ya kiislamu kulingana na taratiu na kanuni za dini hiyo, ila Diva akabisha kwa kauli kwamba yeye ni mwanamke wa kisasa na hawezi vaa nguo za kiislamu siku zote akiwa kazini kama mtangazaji.


 
Hapo ndipo ndoa hiyo ya mahari kima cha milioni 500 pesa za Tanzania bara ilipoingiwa na dosari kwani Sheikh hakuwa tayari kuiasi dini yake kwa sababu ya mwanamke asiyefuata maadili ya kiislamu katika uvaaji.

Wikendi iliyopita baada ya Diva kusombwa na usumbufu wa kuikosa ndoa yake ambapo tayari alikuwa ameikumbatia na mpaka kubadilisha jina lake kwa kuliongeza lile la Abdulrazak, aliamua kuweka mikogo pembeni na kumuomba samahani Abdulrazak Salum kupitia Instagram yake akimuahidi kwamba atakubali kuwa chini yake kwa gharama yoyote ile mradi tu kuitunza heshima ya ndoa.

“Nitaishi katika misingi yako, na kufuata sheria za dini, na nitakua mke chini yako. Diva atakua Diva akiwa nje, ila kwako nitakua mke mbele ya mume wake @sheikh_abdulrazak_salum,” aliandika Diva thee Bawse.

Kauli hii yake ya kunyenyekea na kuonekana kubadili msimamo wake ilipokelewa kwa njia mbalimbali na watumizi wa mitandaoni, baadhi wakimpongeza kwa kutambua umuhimu wa ndoa na kujirudi kwa kujitambua jinsi wanawake wanavyostahili kuishi na kudumu katika ndoa huku baadhi wakimsimanga kwa kujinyenyekesha kwa kiasi hicho kwa mwanaume ambaye tayari ameonesha nia ya kumuacha.

“Hivi ndio mke anavyotakiwa mume atakua juu hyo ndo misingi tulofundishwa na mtume wetu Muhammad,” aliandika shabiki mmoja kwa jina Skygold Tz.

Baadhi walimuambia alikimbilia ndoa akifikiria ni jambo rahisi pasi na kujua kwamba ukifikwa ukweni unafaa kuchukua maagizo ya huko na kuyasahau ya kule ulikotoka na kwamba msamaha wake wa kusema kwamba atakuwa Diva akiwa nje ila ndani atakuwa mke ni kama zile hekaya za kuomba shuka wakati tayari kushakucha kulichele alfajiri ndege wanarindima sauti za kumtukuza muumba wao.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments