Ticker

6/recent/ticker-posts

Harmonize Anamuoa Kajala Mke wa Mtu...Historia ya Kajala Ipo Hivi


Mwijaku; ni mtangazaji na msemaji wa mastaa mbalimbali Bongo akiwemo Harmonize ambapo naye ameingilia mjadala mzito unaosambaa mitandaoni kuwa, jamaa huyo yupo mbioni kumuoa mwanamama Kajala Masanja ambaye ni mke wa mtu kwa sababu hakupewa talaka na aliyekuwa mumewe, Faraji Agustino.

Hii ni baada ya tukio kubwa alilolifanya Harmonize la kumvisha Kajala pete ya uchumba pale Serena Hotel jijini Dar, wikiendi iliyopita.

Data zilizo kwenye makabrasha ya Gazeti la IJUMAA WIKIENDA zinaonesha kwamba baada ya Kajala Kuachana na prodyuza P Funk Majani, bila kupoteza wakati aliolewa kwa ndoa ya kanisani kabisa.

Mjadala mkali unasema kuwa, Faraji Agustino bado ni mume halali wa Kajala kwa sababu walipoachana hakumpa talaka.

Iko hivi; Faraji alipopata kesi ya utakatishaji wa pesa, Kajala alijikuta mikononi mwa Takukuru baada ya kuuza nyumba iliyowekewa kizuizi cha kuuzwa ndipo naye akachanganywa kwenye kesi ya mumuwe.

Hukumu ya kesi hii ilitoka kwa Kajala kufungwa miaka 5 jela au faini ya shilingi milioni 13 ambapo alilipa faini hiyo baada ya kupewa nguvu na Wema Sepetu.

Faraji alihukumiwa kifungo cha miaka 7 jela au faini ya shilingi milioni 200 ambazo alishindwa kuzilipa. Hivyo alitumikia kifungo jela hadi mwaka 2017 alipoachiwa huru.

Baada ya Faraji kutoka jela hakuweza kuendelea kuwa na Kajala, lakini hakumpa talaka.

Kwa mujibu wa ndoa za kikristo, mkioana ndiyo, basi tena mpaka Mungu awatenganishe, sasa baadhi ya watu wanajiuliza Harmonize anamuoa vipi Kajala ilihali hajapewa talaka?

Taarifa za ndani zinadai kuwa, Harmonize ndiye amekubali kubadili dini kutoka kuwa Muislam na kuwa Mkristo wa madhehebu ya Kanisa Katoliki huku akitambulika kwa jina la Robert na alishuhudiwa akipiga ishara ya msalaba baada ya kumvisha Kajala pete ya uchumba.

Sasa; kuhusu Kajala kuwa mke wa mtu, Mwijaku anafafanua anachokijua; “Kwa imani yetu sisi Waislam tuna namna mbili za kuoa. Namna ya kwanza mwanaume anaruhusiwa kuoa hadi wanne.

“Kwa Wakristo ndoa inavunjika kwa vitu viwili; kwa mwanaume kutokuhudumia mke na watu wa nyumbani kwake au mke au mume kuwa kwenye kizuizi ndipo ndoa inavunjika.

“Kizuizi kinachozungumziwa ni kile kinachoweza kumfanya mke asipate haki yake ya msingi

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

2 Comments

  1. Yaani kichekesho 😂🤣😂umeshaona wapi superstar anaoa bibi yake, kajala angekuwa hazichomoi angekuwa anampeleka mjukuu kupanda school bus,sijui ndo kujua naniiio ukubwani,

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yaani umeshaona wapi superstar anaoa bibi yake, Paula angekuwa hazichomoi angekuwa anampeleka mjukuu kupanda school bus 🤪🤪

      Delete
Emoji
(y)
:)
:(
hihi
:-)
:D
=D
:-d
;(
;-(
@-)
:P
:o
:>)
(o)
:p
(p)
:-s
(m)
8-)
:-t
:-b
b-(
:-#
=p~
x-)
(k)