6/04/2022

Kisa Berkane, Mayele atoa masharti Yanga

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


MABOSI wa Yanga wanakuna kichwa baada ya Waarabu wa RS Berkane ya Morocco waliobeba taji la Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu kutuma ofa nono, ili kumnyakua Fiston Mayele ambaye bado wanahitaji huduma yake huku naye akiwapa masharti mazito ili kusalia kikosini.

Berkane inayonolewa na kocha wa zamani wa AS Vita ya DR Congo aliyowahi kuichezea Mayele mwenye mabao 14 na asisti tatu katika Ligi Kuu Bara kwa sasa, Florent Ibenge, inamhitaji straika huyo ili kuimarisha kikosi chao kwa msimu ujao wa michuano.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Yanga kimeliambia Mwanaspoti, Mayele ameuambia uongozi ili aweze kuendelea kubaki Jangwani ni lazima aongezewe mkataba na marupurupu kwenye mshahara wake wa sasa. Mayele kwa sasa ana mkataba uliosaliwa na mwaka mmoja.

“Ofa ni kweli ipo na sisi bado tunamhitaji kutokana na mafanikio aliyotupa ndani ya mwaka mmoja alioitumikia Yanga baada ya kumwambia hivyo ameutaka uongozi umuongeze mshahara na mkataba wa mwaka mmoja ili abaki kuwa na miwili tena,” kilisema chanzo hicho na kuongeza;


 
“Mchakato wa makubaliano mapya bado haujaanza tunasubiri mwisho wa msimu kabla ya mchjezaji hajaondoka kwenda mapumziko, kujiandaa na msimu mpya.

Chanzo hicho kilisema kuna uwezekano mkubwa wa kukubaliana na ofa za Mayele kutokana na umuhimu wake kwenye timu, ukizingatia mbele kuna michuano ya CAF.

“Ndani ya misimu minne mfululizo tumevunja timu kwa kusajijli sajili wachezaji hilo hatutaki lijirudie msimu huu tutafanya kila mbinu kuhakikisha wachezaji muhimu wanabaki na tutaongeza wengine ili kukiboresha zaidi kikosi,” kilisema chanzo hicho.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger