6/02/2022

Menina Afunguka Kilichotokea Mahakamani Mpaka MWIJAKU Kushinda "Niliambiwa Hukumu yake ni ya Siri Sitakiwi Kufika"

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

 


Ameandika @meninalegria kupitia ukurasa wake wa Instagram.

"Nimefika mahakamani leo na hatimae nimekatazwa kuingia kwenye chumba cha hukumu nimezuiliwa kabisa kuingia nakuambiwa kwamba hukumu yake ni ya siri ikiwa mara ya mwisho kwenda mahakamani niliambiwa nifike siku ya hukumu yake huo usiri umetokea wapi?, ikiwa kesi inafahamika na mimi ndio nilifungua mashtaka na hatimae jamhuri kushikilia kesi.

Najiuliza ni kwanini woote walitahamaki kuniona pale mahakamani na kumuuliza wakili wangu kwanini Menina amekuja? Menina hakutakiwa kuja leo hukumu ni ya siri, hivi kweli inaingia akilini yaani nisifike kujua hatima ya kesi kweli?, ikiwa kwa kumbukumbu zangu nilipewa muongozo makamani kwamba inatakiwa nifike siku ya hukumu yake.

Mimi namuachia Mungu kama binaadam hakunipa haki yangu inshaallah nitaipata kwa Mungu kwa kua yeye ndio hakimu wa haki Alhamdulillah Alaakullihal....."

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger