6/02/2022

Wezi Wavunja Kanisa na Kuiba PESA za Sadaka

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Polisi Kaunti ya Kericho nchini Kenya wanachunguza tukio la wizi lililotokea kanisani baada ya Watu wanaodaiwa kuwa ni wezi kuvamia Kanisani katika makazi ya Wachungaji wa Parokia ya Litein na kuharibu mali pamoja na kuiba pesa kiasi ambacho bado hakijabainishwa.

Wezi hao walivamia eneo la Kanisa katika Parokia ya Kikatoliki ya Mtakatifu Mark siku ya jumanne usiku wakati Wachungaji wakiwa wamelala kulingana na ripoti kutoka kwa DCI Kenya.

Taarifa kutoka kwa mmoja wa Maparoko Kanisani hapo aliyejulikana kama Paroko Fr Moses Langat ameeleza kuwa wezi hao waliingia Kanisani na kuharibu mali na vifaa vya kuendeshea ibada pamoja na vyombo vilivyotumiwa kuhifadhi Ekaristi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger