Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla Asimama na Kumtetea ‘Ashura’

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amemtetea mwanamke anayefahamika kwa jina la Ashura wa Tabata kuwa hakuwa mtekaji kama alivyoelezewa hapo awali baada ya Diwani Rwakatare kupatikana kwake.


Makala ameyasema hayo katika kikao cha baraza la Madiwani Halmashauri ya Kinondoni alipohudhuria Ijumaa Juni 24, 2022 wakati walipokutana kujadili ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).


Makalla amesema Ashura anayedaiwa kumteka Rwakatare  aliwasiliana naye wiki moja kabla ya tukio hilo kutokea.


“Ashura mimi namfahamu kwa kuwa alikuwa mke wa rafiki yetu Macheni lakini baada ya mumewe kufariki aliolewa huko Ujerumani,” alisema Makala.


Aliongeza, “Alinipigia simu wiki moja kabla ya tukio kunieleza masuala yake binafsi ya kurudi nchini akitokea Ujerumani na kuna msaada alikuwa anahitaji kutoka kwangu. Hata hivyo,  mara baada ya tukio la Mutta kutokea na kupiga simu kuona namba inayotokea ni yake Ashura ilibidi  nimuhoji kulikoni kufanya hivyo na alinielezea yote na kubaini hakuwa mtekaji kama watu wanavyosema.”


Mradi uzalishaji nyama bora wazindulia

“Yule ni rafiki wa familia ya kina Mutta  na hata walipomnasa Mutta walimkuta ndio amempa supu ya kuku,” alimaliza kueleza Makalla.


Naye Diwani wa Kawe (CCM), Mutta Rwakatare, alipopewa nafasi na Mkuu wa mkoa kuzungumza aliahidi kikao cha baraza la madiwani halmashauri ya Kinondoni kuwa hatopotea tena.


“Kwanza nikushukuru mkuu wa mkoa. Pia nitumie kikao hiki kuahidi kwamba sitapotea tena kwani nilikuwa kwenye ‘Royal Tour’ ya Lost and Found.”

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad