6/10/2022

Mtoto wa Miaka 10 Amuua Adui wa Mama yake

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPAMtoto mwenye umri wa miaka 10 kutokea jimbo la Florida nchini Marekani amekamatwa na kushtakiwa kwa kosa la mauaji ya Mwanamke aliyehusika katika ugomvi na mama yake.

Idara ya Polisi ya Orlando ilimchukua Mtoto huyo na kumuweka chini ya ulinzi kwa tuhuma za mauaji ya daraja la pili na kumpeleka kwenye kituo cha Watoto watukutu.

Mauaji ya Lashun Rodgers (41) anayeonekana kwenye picha kushoto yalitokea May 30, 2022 wakati akigombana na Mama wa mtoto huyo, Lakrisha Isaac (31) anayeonekana katikati kwenye picha katika apartment nchini humo ambapo Mtoto huyo alichukua bunduki ya mama yake na kufyatua risasi mbili, polisi wamesema.

Lashun alipelekwa hospitali lakini alifariki baadae ambapo Mama wa mtoto huyo alikamatwa muda mfupi baada ya tukio na anakabiliwa na mashtaka mengi ikiwemo kuua bila kukusudia, shambulio la kikatili kwa kutumia bunduki na kutelekeza mtoto
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger