"Huenda Nisipate Watoto" Mbosso Afunguka Kuhusu Tatizo Kubwa la Moyo Linalomuathiri

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Staa wa Bongo Mbwana Yusuf Kilungi almaarufu Mbosso amefunguka kuwa anakumbwa na matatizo makubwa ya moyo.

Msanii huyo wa WCB mwenye umri wa miaka 29 amefichua kuwa amekuwa akipambana na hali hiyo kwa kipindi kirefu.

Akiwa kwenye mahojiano na Wasafi Media, Mbosso alieleza kuwa hali hiyo inayofanya mwili wake kutetemeka imesababishwa na kuziba kwa mishipa yake.

"Nimeambiwa matatizo yangu yanatokana na mishipa yangu ya damu kuzibwa na mafuta. Hali hii haijanipata ukubwani, ni tangu nizaliwe," Mbosso alisema.


Mwanamuziki huyo alifichua kuwamara nyingine hali hiyo husababisha ganzi mwilini mwake kiasi kwamba anapoteza hisia.

Mbosso alisema ugonjwa upo ndani ya familia yake na amekuwa nao tangu kuzaliwa kwake. Alisema kuwa hata hivyo kuna nuru gizani kwani tayari kuna mpango wa hali hiyo kuenda kurekebishwa ughaibuni.

"Nimesisitizwa nifanye mazoezi. Kuna wataalamu pia niliwasiliana nao. Natakiwa nisafiri kwa ajili ya kuenda kupatana nao," Alisema.


Mbosso alisema atasafiri kuenda kutibiwa baada ya kupanga mambo yake nyumbani kwani matibabu yake yatachukua muda mrefu.

Alifichua kuwa anasaka matibabu kwani madaktari waliwahi kumwarifu kuwa ugonjwa wake huenda ukamsababishia utasa baada ya kutimiza miaka 30.

"Daktari aliniambia shida yangu huenda ikawa kubwa zaidi baada ya kufikisha miaka 30. Alisema huenda ikanipelekea nisipate tena watoto nisipofanya matibabu," Alisema.

Mwanamuziki huyo pia aliweka wazi kwamba sio wengi ambao wamekuwa wakifahamu kuhusu ugonjwa wake.


Alifichua kwamba ni wazazi wake tu, baby mamas wake na bosi wake Diamond Platnumz ambao wamekuwa wakijua kuhusu hali hiyo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad