6/01/2022

Rais Samia Azindua Kitabu cha Mwanamuziki Sugu Nguli wa Hip Hop Tanzania

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan amezindua kitabu cha mwanamuziki nguli wa Hip Hop, Mr 2 maarufu kama Sugu @jongwe__ kiitwacho "Muziki Na Maisha" kwenye tamasha lake la kutimiza miaka 30 katika tasnia hiyo.

Katika tamasha hilo lililoitwa The dream Concert, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe Mohamed Mchengerwa, Katibu Mkuu. Dkt, Hassan Abbasi, Naibu Katibu Mkuu, Saidi Yakubu, watendaji wa Wizara na wadau mbalimbali walihudhuria.

Tamasha hilo lilipambwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali ikiwa ni pamoja na Sugu mwenyewe ambaye alitumbuiza na kukonga nyoyo za mamia ya watu waliohudhuria.

Mhe. Rais amemtunukia tuzo, Sugu huku akimpongeza kuwa miongoni wasanii wenye nyimbo zenye maadili.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger