6/04/2022

Wema Sepetu "Mimi Kuimba Siwezi Sitaki Kujitia Aibu"

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Muigizaji maarufu kutoka kwenye kiwanda cha bongomovie, Wema Sepetu (Tanzania sweetheart) ameweka wazi kuwa hana mpango wa kujitosa kwenye muziki wa Bongofleva kama ambavyo waigizaji wengine walivyojitosa kwenye Muziki mfano Hemedy phd

Hata hivyo, amebainisha kuwa ana uwezo wa kuingiza sauti yake kwenye nyimbo za wasanii wengine

"Mimi huwa napenda kuingiza zile sauti za nyuma, kuimba siwezi, sitaki kujitia aibu, kama wasanii wanapenda sauti zile za nyuma, mimi niko vizuri Hamna wimbo wowote wa Wema unakuja," alisema.

"Sitegemei kuingia kwenye kuimba kwa kweli. Mtanicheka nikianza kuimba, siko tayari," alisema Wema akiongea na Wanahabari hapo juzi.

Alifungua code pia kuwa amewahi kuingiza sauti yake kwenye nyimbo kadhaa za aliyekuwa mpenzi wake, Diamond Platnumz, nyimbo hizo ni ni Lala Salama na Chanda Chema.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger