6/08/2022

Yanga Yamtega Mayele, Yaahidi Kupambana Kufa Kupona Kumlinda

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


UONGOZI wa Yanga, ni kama umemtega mshambuliaji wa timu hiyo, Fiston Mayele baada ya kutenga kiasi kikubwa cha fedha kuhakikisha nyota huyo anabaki kikosini hapo na haendi RS Berkane anapohitajika.

Hivi karibuni, tetesi nyingi za usajili zilimuhusisha mshambuliaji huyo kuhitajika na RS Berkane ya nchini Morocco anayoichezea aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Tuisila Kisinda.

Mayele alijiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu huu akitokea AS Vita ya DR Congo, ambapo ameonesha kiwango kikubwa cha kufunga mabao akiongoza kwa ufungaji Ligi Kuu Bara akiwa nayo 14 sawa na George Mpole wa Geita Gold.

Akizungumza na Spoti Xtra, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, alisema ni ngumu kwao kukubali kumuachia mshambuliaji aina ya Mayele, hivyo wapo tayari kutumia kiwango chochote cha fedha ili wafanikishe malengo yao ya kumbakisha.


 

Yanga imesema ipo tayari kuweka kitita chochote kile kumbakisha Mayele klabuni
Aliongeza kuwa, kikubwa watakachokifanya ni kuboresha baadhi ya mahitaji yake atakayoyataka ili asiondoke kikosini kwao.

“Tunafahamu umuhimu mkubwa wa michuano ya kimataifa, kama yalivyokuwa malengo yetu ni kufika nusu fainali kimataifa, hivyo ni lazima tuwe na kikosi imara kitakachotufikisha huko.

“Hivyo hatutakubali kumuachia mchezaji yeyote muhimu na tegemeo katika timu yetu kuelekea msimu ujao ambao tunaamini ndio utakuwa wenye mafanikio kwetu.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger