6/22/2022

Zuchu "Hakuna Uwekezaji wa Mziki Tanzania Wengi Wenye Vipaji Wako nje ya Tasnia"

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Mwimbaji nyota toka WCB, msanii @officialzuchu ametoa ya moyoni kufuatia namna tasnia ya muziki ilivyo hapa nchini kwa kipindi kirefu na wengi wamekuwa wa hanga kwenye hilo, amebainisha kuwa hakuna uwekezaji wa kutosha katika muziki huku wengi wenye vipaji wako nje ya tasnia yenyewe.


"Ninaamini kuna wasanii wengi wako nje ya tasnia ya muziki wana vipaji kuliko walioko ndani na hiyo ni kwasababu hamna uwekezaji wa muziki nchini mwetu". ameeleza Zuchu kwenye #SalamaNa show ya mtangazaji Salama Jabir.


Kwenye mahojiano hayo pia ameeleza namna alivyoshindwa kufua dafu kwenye shindano la kwanza la karaoke barani Afrika la Tecno Own The Stage nchini Nigeria, nakujiona hajui kuimba hadi alipofikia ndoto zake za kutamani kufanya kazi na @diamondplatnumz @babutale @mkubwafellatmk


"Nilishindwa mashindano ya uimbaji nikajiona sijui kuimba. Mama alinipeleka training kwenye band. Nilimwambia kuwa nilikuwa nataka kufanya kazi na Diamond, Tale au Fella." alimalizia Zuchu.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger