Ticker

6/recent/ticker-posts

Aziz Ki Ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi ya Ivory Coast kwa Msimu Uliopita


KIUNGO mpya wa Yanga, Stephane Aziz Ki ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Ligi ya Ivory Coast kwa msimu uliopita wakati akiichezea Asec Mimosas.

Nyota huyo ambaye amejiunga na Yanga msimu huu usajili wake ulikuwa gumzo kutokana na utambulisho wake uliofanyika Julai 15 alfajiri huku akitegemewa kufanya makubwa na mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara kwa sababu ya kiwango chake kizuri ambacho alionyesha.

Mbali na Aziz Ki ila kiungo mpya wa Azam FC, Tape Edinho ameshinda pia tuzo ya kiungo bora wa msimu wakati akiitumikia klabu ya ES Bafing FC ya kwao Ivory Coast.

Katika tuzo hizo za msimu, Edinho alimshinda nyota wenzake wa Azam, Kipre Junior aliyesajiliwa naye msimu huu akitokea Sol FC ya huko huko Ivory Coast sambamba na nyota mwingine, Djire Abdoulaye anayechezea klabu ya Racing Club Abidjan.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments