Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Siku moja baada ya Kamati ya Maadili ya Shirikisho la soka nchini Tanzania ‘TFF’ kutangaza kumfungia kwa miaka miwili kujihusisha na soka na kumtoza faini ya Shilingi milioni 20, Msemaji wa Young Africans Haji Sunday Ramadhana Manara ametamba kuendelea na shughuli za kuelekea Tamasha la Siku ya WANANCHI.
Kamati ya Maadili ya TFF imebaini Haji alitumia Lugha ya vitisho dhidi ya Rais wa Shirikisho Wallace Karia wakati wa mchezo wa Fainali Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ kati ya Young Africans dhidi ya Coastal Union uliopigwa Julai 02 jijini Arusha, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Manara ametumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kufikisha ujumbe kwa wanachama na mashabiki wa Young Africans huku akiwataka kutokua na hofu dhidi yake kwani atashiriki kwenye Tamasha la Siku ya WANANCHI litakalofanyika Agosti 06, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
Manara ameandika: Kumbe Tatizo ni hili?
Uhhhh lalalaah!!!
Wamebugi kwangu,,,Sitawaacha Wananchi,,na litakuwa Tamasha kubwa kuliko walivyodhamiria.
Simjui yoyote nchi hii anaenisogelea kwa kufuatiliwa ktk Instagram ,kwa Watu wa football na Sports kwa ujumla kunizidi ,,nguvu hyo niliojaaliwa na Mungu,ntaitumia effectively kulipush hili Concert kuu la kisoka,,
Ikiwa Parade yetu ilivunja Rekodi why tushindwe hili?
Msifadhaike hata kidogo,,tuombe uhai tu coz dhulma huwa haina mwisho mwema na always haki hushinda,,ni suala la muda tu
Nb:: Sipoi hata tone na tabu ipo pale pale,,.sanasana ndio itazidi,,otherwise waje kuniua,,
Yanga Bingwa na mm ndio Bugati
Byuti Byuti
Mwisho wa kunukuu ujumbe wa Manara
Jana Alhamis (Julai 21) Katibu wa Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Walter Lungu alisoma hukumu ya Kamati kuhusu shauri lililowasilishwa la Ofisa wa Young Africans anga Haji Manara
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA