Mapya Yaibuka! Meya wa Nchini Mexico Afunga Ndoa na Mamba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Tukio limetokea huko San Pedro ambapo meya huyo kwa jina la Victor Hugo amemuoa mamba huyo mwenye miaka 7. Kabla, alhamisi wiki hii mamba huyo alibatizwa na anatambulika kwa jina la Princess, siku iliyofuata Ijumaa ndio ndoa ikafungwa ambapo bwana hurusi alimbusu mamba huyo mdomoni ingawa mamba alikuwa amefungwa mdomo asije kukinukisha katikati ya sherehe na kujeruhi watu


Watu walikula, kunywa na kusaza huku muziki ukipigwa na watu kuserebuka. Mama mtu mzima kwa jina la Elia ambaye alipewa kazi kuhakikisha harusi hiyo inaenda vizuri, amekaririwa akisema aliumiza sana kichwa kujua mamba huyo bibi harusi atavaa nini lakini hatimaye gauni zuri na shela vilishoneshwa kwa ajili ya mamba huyo na kumpendeza vilivyo


Wanakijiji hawakuishia kula na kucheza muziki tu, bali pia walipata nafasi ya kumbeba na kumshika bibi harusi huyo kwa jina la Princess na kuzunguka nae mitaani kwa furaha


Pamoja na hayo, harusi hiyo ni ya kimila mamba anaolewa ambapo watu wa kijiji husika wanaamini kuwa ni muunganiko wa nguvu za kibinadamu na nguvu za kimungu hivyo wanaamini wavuvi maeneo yao watavua samaki wengi, watavuna mazao mengi, kupata chakula kingi, mvua nyingi kunyesha na kila aina ya neema

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad