Mastaa 6 baibai Yanga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




MASHABIKI wa Yanga bado wanaendelea kushangweka baada ya timu hiyo kubeba mataji matatu, huku wakiendelea kusikilizia mastaa wapya watakaoshuka kikosini kwa msimu ujao, lakini tayari imefahamika beki wa kushoto, Yassin Mustafa anachwa kumpisha Joyce Lomalisa ambaye muda wowote atakuja Jangwani.

Yassin aliyesajiliwa na Yanga misimu miwili iliyopita akitokea Polisi Tanzania, ni kati ya wachezaji sita ambao watapewa mkono wa kwaheri Jangwani na nafasi yake itachukuliwa na Lomalisa aliyesajiliwa kutoka DR Congo.

Habari za kuamini kuwa ndani ya Yanga, zinasema Yassin ni kati ya wachezaji sita wa kikosi cha sasa watakaotemwa akiwamo Chico Ushindi ambaye awali ilielezwa huenda angebakishwa kwa kazi kubwa aliyoifanya mwishoni mwa msimu na kumfurahisha Kocha Nasreddine Nabi anayetuliza akili kwa sasa katika Mbuga ya Serengeti pamoja na familia yake.

Mbali na nyota hao wengine ambao hawatakuwa kwenye kikosi hicho kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika ni Heritier Makambo, Paul Godfrey ‘Boxer’, Deus Kaseke, Mapinduzi Balama na Yacouba Songne atakayetolewa kwa mkopo kama tulivyodokeza katika gazeti la jana.

“Yassin ni kati ya wachezaji watakaotemwa kwa msimu ujao, akiwamo Chico na Makambo, wengine wameshataarifiwa na wameanza kujiunga na timu nyingine kama ilivyo kwa Boxer,” klilisema chanzo hicho kilichofichua kuwa, wikiendi hii, kiungo Gael Bigirimana atatua nchini na kutambulishwa kwenye Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa klabu hiyo unaofanyika Jumamosi.

Mbali na Gael aliyewahi kupita Coventry City, Newcastle United na Rangers, pia Stephane Aziz KI naye atakwepo kwenye mkutano huo, wakati Lomalisa ikielezwa anasubiri kujiunga kambini.


----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad