Ticker

6/recent/ticker-posts

Mayele Ana Thamani zaidi Tanzania

 


Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya klabu ya Yanga, Eng.Hersi Said amemtaja mshambuliaji Fiston Mayele kuwa mchezaji mwenye thamani kubwa zaidi kwenye Ligi Kuu NBC Tanzania iliyomalizika msimu wa mwaka 2021-2022.

Akizungumza na EATV, Eng.Hersi amesema  ubora na uwezo mkubwa aliounyesha Mayele umemfanya ajijengee umaarufu mkubwa kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.


“Mayele ni mchezaji mzuri hata ubingwa huu umechangiwa na juhudi zake katika timu yetu, hivyo hakuna mchezaji yoyote wa kulinganishwa na straika huyo'' amesema Mjumbe huyo wa Kamati ya Mashindano ya Yanga Eng.Hersi Said.


Yanga ambao ni mabingwa wapya wa Ligi kuu msimu 2021 – 2022 huku Ligi kuu soka Tanzania Bara itarajiwa kuanza Agosti 17 mwaka huu na kumalizika Mei 27 ,2023

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments