Mjue Mugalu Ana Ofa Nne Mezani Kwake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPAMSHAMBULIAJI wa Simba, Chriss Mugalu ameondoka nchini na kwenda kwao DR Congo huku akiwa hafahamu hatma yake ya msimu ujao kutokana na mvutano unaoendelea ndani kwa mabosi wake.

Hata hivyo, Mwanaspoti linajua Mugalu ana ofa za timu nne mkononi anazunguka nazo ambazo mabosi wake ndiyo wataamua kwani bado ana mkataba na Simba.

Miongoni mwa timu zilizoonyesha nia hiyo ni Zesco United, Nkana Red Devils, Power Dynamos zote za Ligi Kuu Zambia pamoja na FC Saint-Eloi Lupopo inayoshiriki Ligi Kuu DR Congo.

Mugalu alipojiunga Simba Agosti 2020, akitokea Dynamos alisaini mkataba wa miaka miwili ambao ndani yake ulikuwa na nyongeza ya mwaka mmoja na kuwa mitatu ambao sasa umebaki mmoja.


Mugalu ana mkataba Simba lakini kuna mvutano unaoendelea kwani baadhi ya viongozi wanataka waachane naye kutokana na kiwango chake msimu uliopita kuwa chini huku wengine wakitaka apewe muda zaidi.

Mugalu hakufanya vizuri msimu huu kutokana na kuwa na majeraha ambapo amemaliza ligi bila kufunga bao hata moja katika mechi alizopata nafasi ya kucheza tofauti na msimu uliopita akimaliza na mabao 15.

Alipotafutwa Mugalu alisema ameenda kwao kwa ajili ya mapumziko ila bado ana mkataba na Simba unaomalizika msimu ujao huku akidai kama kuna ishu nyingine basi si rasmi.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad