Ticker

6/recent/ticker-posts

Rais Biden Akutwa na Covid-19, Taarifa Yatikisa Ikulu ya Marekani
RAIS wa Marekani Joe Biden ameripotiwa kukutwa na maambukizi ya Virusi vya Covid-19 hiyo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Marekani.


Rais Biden alikuwa tayari ameshatumia dozi mbili za kujikinga na Covid- 19 aina ya Pfizer muda mchache kabla ya kuingia madarakani ambapo chanjo ya kwanza alichanja mwezi Septemba 2021 na ya pili alichanja mwezi Machi mwaka huu.

 

“Asubuhi ya leo Rais Biden amekutwa na maambukizi ya virusi vya Covid-19 na amechanjwa vizuri ingawa amekumbwa na dalili za maambukizi ya virusi hivyo.” Alisema Msemaji wa Ikulu Karine Jean –Pierre.


Biden aripotiwa kukutwa na maambukizi ya Virusi vya Covid-19

Kwa muda mrefu Ikulu ya Marekani imekuwa ikiendesha shughuli mbalimbali zinazohusisha mikusanyiko ya watu pasipo kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya Covid-19.

 

Aidha mnamo Aprili 30, 2022 Rais Biden alihudhuria shughuli yenye mkusanyiko wa watu wengi katika Ikulu ya WhiteHouse akiwa hana tahadhari yoyote ya kujikinga na maambukizi ya Uviko -19 na kusema kuwa anatambua hatari ya virusi hivyo lakini lilikuwa ni jambo la thamani kwa yeye kushiriki katika tukio hilo.

 

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments