Umeme Vijijini si kwa Ajili ya Kuwasha Taa Pekee – Makamba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Waziri wa Nishati January Makamba wakati ametembelea Kiwanda cha Kuza Afrika cha Kuchakata maparachichi kilichopo Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya
WAZIRI wa Nishati, January Makamba ameeleza kuwa Serikali haipeleki umeme vijijini kwa ajili ya kuwasha taa pekee bali kuchagiza pia shughuli za kiuchumi ikiwemo uanzishaji  wa viwanda.

Amesema hayo baada ya kutembelea kiwanda kinachochakata  parachichi  ili kutengeneza mafuta  cha KUZA AFRIKA kilichopo wilayani Rungwe Mkoa wa Mbeya mbacho  kimeunganishiwa umeme na TANESCO.

Makamba amesema kuwa, uwepo wa Kiwanda hicho  ni matokeo ya uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali katika sekta ya Nishati ambao umezaa matunda kwani kiwanda hicho pamoja na kuongezea thamani  mazao ya Wakulima, kimezalisha ajira zaidi ya 200 ndani ya kiwanda na katika mashamba ya parachichi.


Wafanyakazi wa Kiwanda cha Kuza Afrika kinachochakata maparachichi wakiwa kazini
Ameongeza kuwa, msingi mzima wa kupeleka umeme vijijini ni kusawazisha maendeleo kati ya watu wa vijijini na mijini kwani shughuli za kiuchumi kama za viwanda zinaboresha pia uchumi wa wananchi wa vijijini.


 
Meneja wa TANESCO, Wilaya ya Rungwe, Mhandisi Mukhsin Kijemkuu amesema kiwanda  hicho kabla ya kufungiwa transforma yake kilikuwa kikizalisha lita 2000 kwa siku lakini baada ya kupata Transfoma wiki moja iliyopita kitazalisha lita 4000 kwa siku.


Zao la Parachichi linaongezewa thamani katika Kiwanda cha Kuza Afrika kilichopo Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya
Ameongeza  kuwa kwa lita 4000 zinazotarajiwa kuzalishwa kwenye kiwanda hicho mwekezaji angetumia shilingi milioni 50 kununua dizeli ya kuendesha mitambo ila kwa kuwa sasa anapata umeme wa kutosha  atatumia takriban shilingi milioni 30.

Pamoja na kuishukuru Wizara ya Nishati kwa kutenga fedha za kupeleka umeme kwenye maeneo kama hayo amekaribisha wawekezaji wengine kuwekeza kwenye miradi kama hiyo kwani hali ya upatikanaji umeme sasa imeimarika na pia TANESCO Itaongeza mapato yake
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad