Zaidi ya Watoto 358 Waripotiwa Kuuawa Kwenye Vita ya Urusi na Ukraine

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa


RIPOTI mpya ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Ukraine imebainisha kuwa jumla ya watoto 358 wameripotiwa kuuawa katika vita inayoendelea nchini humo dhidi ya taifa la Urusi.


Kwa mujibu wa mtandao wa The Kyiv Independent mbali na vifo vya watoto 358, jumla ya watoto wengine 681 wameripotiwa kujeruhiwa tangu kuanza kwa vita hiyo Februari 24, 2022.


Vifo vingi vya watoto vimeripotiwa kutokea katika Jimbo la Donetsk


Ofisi ya Mwanasheria Mkuu imebainisha kuwa namba kubwa ya wahanga wa watoto hao imetokea katika mji wa Donetsk ambapo jumla ya watoto 361 wameripotiwa kuwa aidha wameuawa au wamejeruhiwa.


Vita kati  ya Urusi na Ukraine ilianza Februari 24, 2022 ambapo hadi sasa mapigano bado yanaendelea huku kukiwa na taarifa kuwa Ukraine ipo katika hali mbaya ya uhaba wa chakula kutokana na Urusi kubeba asilimia kubwa ya nafaka zinazozalishwa nchini humo na kusafirishwa kupelekwa Urusi

_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad