Afisa Habari wa Klabu ya Yanga Hassan Bumbuli Ametangaza Rasmi Kumalizana na Timu Hiyo

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPAAfisa Habari wa Klabu ya Yanga Hassan Bumbuli ametangaza rasmi kumalizana na timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Jangwani.

Kupitia ujumbe wake kwa wanahabari Bumbuli amewashukuru kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi chake chote.

“Ndugu zangu, naomba kutumia fursa hii, kuwashukuru kwa ushirikiano wenu katika kipindi chote nilichokuwa Afisa Habari wa Klabu ya Yanga.”

“Nawaaarifu rasmi kwamba nimemaliza mkataba wangu wa kuitumikia timu ya Yanga na sasa narejea kwenye majukumu yangu mengine.”

“Nawashukuru sana kwa Umoja wenu, ushirikiano wenu katika kipindi chote tulipokuwa pamoja.”

Mpaka sasa Mrithi wa Hassan Bumbuli katika kitengo cha Afisa Habari ndani ya Yanga hajatangazwa.


Unapenda Simulizi za Kusisimua?

Kuna Simulizi ya NDOA YANGU na kuna INATOSHA, Zitakukosha sanaa.
Bofya HAPA kufurahia sehemu ya 1 bure ndani ya group la telegram.


 

 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad