Alikamwe "Mambo 10 Nilioyaona POLISI vs YANGA...Mechi Dume Iliyoamuliwa Kiume""1: MABINGWA WAMEANZA NA POINTI 3 za KIBINGWA👊 Mechi Dume imeamuliwa kiume. Si rahisi kufanya ‘Comeback’ mechi 2 mfululizo kama huna wachezaji wenye sifa ya Upambanaji✊

2: Polisi walikuja kuwapa Yanga swali moja ngumu Uwanjani. Sisi Tutawaonyesha Tutakaba na nyie Tuonyesheni sanaa yenu ya kushambulia..

3: Polisi walikuwa kwenye umbo la 4-5-1 wakiiweka Timu kwenye ‘Mid Block Defensive System’. Ikawa rahisi kwao kufanikiwa kutokana na mpango wa Yanga katikati ya kiwanja! How?

4: Yanga walikwenda na 4-3-3, wakitaka kupambana na changamoto ya pitch kwa kushambulia mapana ya uwanja. Utatu wao kwenye safu ya kiungo ulijaa maarifa Lakini changamoto ikawa kasi

5: Timu inayokaba na watu 7-9 ikaenjoy zaidi ikicheza dhidi ya viungo wanaopiga pasi sana. Bigirimana & Aucho wakawa wanacheza chini na Eneo la Tatu ya mwisho ya Polisi na Faida ya Idadi ya namba ikawa kwa Polisi pindi wanapozuia

6: Again.. NABI AMESHINDA mechi kwenye Sub yake. Alisoma tatizo na akaja na suluhisho. ‘Sub’ ya akili zaidi ni ile ya kumtoa Bigirimana na kumpeta Feisal. Kasi ikaongezeka na Yanga wakaanza kushambulia kwa idadi kubwa kwenye eneo la mwisho

7: Mayele ni mfungaji mzuri. No doubt kwenye hilo Lakini when it comes to kusaka pointi 3 muhimu, pigo la penalti ni vyema likaachwa kwa Djuma Shabani.

8: Well Done Salum Ally Kipemba na Hamis Kanduru👏 Uwezo wa kukokota mpira uliwapa nguvu sana Polisi kwenye Quick Positive Transition! Walipochoka, Timu ikakata. Na ni kama Benchi alikosekana mchezaji mwenye Quality ile

9: AZIZ KI anajua sana mpira. Changamoto yake imeonekana kwenye Fitness. Well Done Moloko👏 Ameendelea kuthibitisha kwanini alistahili kubaki Yanga msimu huu

10: Lomalisa anatakiwa kujiimarisha zaidi. Iddy Kipwagile pia. Polisi wanatakiwa kusajili haraka straika asilia kwenye kikosi chao

Nb: Wameumia Polisi mpaka Mgambo wa Kariakoo 😂

💥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

💥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

💥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad