Breaking News: Mgombea Urais wa Kenya Raila Odinga Afunguka Kukataa Matokeo ya UraisMgombea Urais wa Kenya kwa tiketi ya Azimio la Umoja Raila Odinga ameongea leo kwa mara ya kwanza kupitia vyombo vya habari baada ya jana Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi kutangaza Mshindi wa Urais kuwa ni William Ruto.


Raila amesema “nawashukuru Wakenya wenzangu walioshiriki uchaguzi, nawashukuru Wafuasi wa AZIMIO kwa kutofanya fujo au kujichukulia hatua mkononi baada ya matokeo kutangazwa na ninawaomba waendelee kuwa watulivu”


“Sisi tunapenda amani, Yule Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi amepindua matokeo na kutengana na wenzake, hatutakubali Mtu mmoja ajaribu kuleta vurugu na kubadilisha kila kilichoamuliwa na Wakenya, Mungu ibariki Kenya Nchi yetu, tutawatangazia hatua zaidi hapo baadaye” ——— amesema Raila Odinga.


đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

đŸ’¥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad