Ajali Yaua Watatu Handeni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Handeni. Watu watatu wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya basi la Burudani kuligonga lori lililokuwa limeegeshwa katika kijiji cha Taula kata ya Kwedizinga wilayani Handeni mkoani Tanga.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Septemba Mosi 2022, saa moja usiku ambapo basi la kampuni ya Burudani liligonga lori lililokuwa limeharibika barabarani, baada ya dereva wake kushindwa kulipita kutokana na mbele yake kuwepo gari nyingine.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, David Chidingi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa chanzo cha ajali ni mwendo kasi, ambapo dereva alilishindwa gari lake na kuligonga lori kwa nyuma.

Ameongeza kuwa katika ajali hiyo watu wawili wamekufa hapo hapo huku mmoja akifariki akiwa anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya Korogwe Magunga.


"Waliofariki na kujeruhiwa wote ni wanaume lakini chanzo cha ajali ni mwendo kasi, dereva wa basi alikuwa kasi na kushindwa kufunga breki alipofika eneo hilo ambalo kulikuwa na lori mbele yake lililoharibika na kuligonga kwa nyuma," amesema Kamanda Chidingi.

Mkuu wa wilaya ya Handeni, Siriel Mchembe aliyefika katika eneo la tukio amesema, changamoto ya eneo hilo ni jembamba hivyo ikitokea changamoto ya gari kuharibika inakuwa ni shida kwenye kupishana hivyo kusababisha ajali.

"Niombe sana Tanroads muangalie ni jinsi gani mtaweza kuongeza upana wa barabara hii hasa hili eneo ili madereva waweze kupishana hata kama kuna dharula maana hapa ni eneo ambalo kunatokea ajali mara kwa mara," amesema Mchembe.


Shuhuda wa ajali hiyo, Hemedi Rashid amesema majira ya saa mbili kasoro walisikia kishindo kikubwa na walipofika eneo la tukio walikuta ni basi limegonga lori.

Ameongeza kuwa eneo hilo ajali hutokea mara kwa mara hivyo kuomba serikali kuangalia ni jinsi gani wataweza kuthibiti mwendo kasi wa madereva.

Waliofariki kwenye ajali hiyo ni Saidi Mohamed utingo, Willy Jackson na marehemu wa tatu jina lake bado halijajulikana.

Aidha majina ya majeruhi yaliopatikana awali kwenye ajali ni Khalifan Msoka mkazi wa Korogwe, Nyange Hubert na Frank Komba wote wakazi wa wilaya ya Moshi.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad